Chidi afunguka picha za ujauzito wa Lil Nas

Ijumaa , 10th Sep , 2021

Rapa Chidi Benz amefafanua post yake aliyoshea kwenye mtandao wa Instagram baada ya kupost picha za ujauzito wa Lil Nas x wa Marekani kwa kusema watu wanafanya kiki kwenye vitu vilivyopitiliza.

Kushoto ni Chidi Benz kulia ni Lil Nas x

Akizungumzia kuhusu picha hiyo Chidi Benz anasema amepost kwa maana ya kuwakumbusha baadhi ya wasanii wa Bongo wanaofanya kiki kama hizo.

"Instagram yangu kuna mtu anaiongoza ila ile picha ya Lil Nas akiwa mjamzio niliipost mimi, nilikuwa naona ni jinsi gani watu wanatafuta kiki iliyopitiliza pia nilikuwa nawaongelea wa hapa nyumbani ​achana na hao ambao wanajichagulia na hawapo duniani".