Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Chid Benz bado una nafasi - Kalapina

Jumanne , 27th Sep , 2016

Msanii Kalapina ambaye pia ni mwanaharakati wa kupambana na madawa ya kulevya na akiwa mmoja wa watu waliomsaidia Chid Benz baada ya kuathiriwa na madawa ya kulevya, amefunguka kuhusu hali ya sasa ya msanii huyo.

Kalapina (Kushoto), Chid Benz Benz (Kulia)

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka 'sober house', hivyo amemtaka kurudi na kuwasikiliza watu waliomsaidia ili asifikie pabaya.

“Chid Benz hakumaliza muda wa matibabu alivyotoka 'sober house' ndani ya siku 28, kwahiyo mi namuomba afikirie faida alizozipata sober na faida anazozipata sasa hivi akiwa mtaani, nafasi bado ipo kwake kwa sababu tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa, kwa hiyo anatakiwa atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza kujisahihisha”, alisema Kalapina.

Kalapina aliendelea kutufungulia na yale ambayo yalikuwa hayajifika kwenye vyombo vya habari kuwa msanii huyo (Chid Benz) na msanii Ray C ambaye pia ni muathirika na madawa ya kulevya, walipata wafadhili wa kuwapeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kitendo hicho.

“Kulikuwa kuna safari ya yeye na Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa matibabu zaidi, lakini ilitakiwa subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka kukaa sober anataka kukaa mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena ku'invest hela yao inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina.

Pia Kalapina amekanusha suala la kwamba walimtelekeza msanii huyo, kwani walikuwa wanakwenda kumtembelea na kumpelekea mahitaji yote muhimu.

Msikilize hapa:-

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea