Jumatatu , 5th Mei , 2014

Baada ya kushinda tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki kutoka katika tuzo kubwa za muziki za KTMA, Jose Chameleone ambaye amekuwa Tanzania kwa siku kadhaa sasa, amekimwagia Kiswahili, lugha ambayo imemfanya kueleweka Afrika Mashariki.

Chameleone ambaye ameshinda tuzo hiyo kupitia ngoma yake ya Tubonge, amefanikiwa kujizolea mashabiki mbalimbali kutoka nchi hizi za Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba katika lugha ya Kiingereza, Kiswahili na Kiganda.

Msanii huyu amesema pia kuwa anashukuru sana kwa kuweza kushinda tuzo hii mfululizo kutokea mwaka 2012, dalili inayyonyesha kuwa Afrika Mashariki inafurahia kazi zake anazozifanya kwaajili ya kuwaburudisha.

Tags: