"Cha kwanza ni IG, Benki atajua mwenyewe" - Idris

Alhamisi , 29th Apr , 2021

Mchekeshaji na muigizaji Idris Sultan amehoji kuhusu baadhi ya mastaa na watu wa kawaida kuwaza kuwafungulia watoto wao akaunti za mtandao wa Instagram lakini wanasahau kuwafunguluia akaunti za Benki.

Picha ya Idris Sultan

Idris Sultan amehoji taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo ameandika kuwa  

"Siku hizi tukipata watoto tu cha kwanza ni IG Account, Bank Account atajijua mwenyewe, 'likes' za ndugu zetu zitawasomesha nadhani, hapo tunawapa presha kuwa ni lazima kuiendeleza hiyo 'page' wakikua, itakuaje kama hawataki mitandao ya kijamii wanataka kuwa maspai".

Aidha baada ya post hiyo msanii mkongwe wa HipHop AY, nae alishea comment kuhusiana na hilo kwa kuandika "Halafu Akaunti ya mtoto ina-post 'i love you dad' pia una-comment 'i love you too son au daughter' ni ujinga".