Jumanne , 1st Jul , 2014

Msanii maarufu wa miondoko ya R&B wa nchini Rwanda Bruce Melody anazidi kuiwakilisha nchi yake Afrika Mashariki ambapo hivi sasa mkali huyo ameachia wimbo mpya na msanii kutoka kundi la Goodlyf nchini Uganda, Mowzey Radio.

Wasanii Mose Radio na Bruce Melody

Baada ya kufanya colabo na wasanii mbalimbali nchini Uganda wakiwemo pia Jamal na Fille, Bruce ameelezea kuwa hivi sasa anatarajia kufanya kazi zaidi na wasanii kutoka Afrika Mashariki ili kukuza zaidi muziki wake.

Bruce amekuwa ni moja ya wasanii ambao wanapenda kuwapa moyo wasanii mbalimbali nchini humo kufanya muziki wao live stejini.