Msanii wa muziki Bobi Wine wa nchini Uganda
Msanii huyo amechaguliwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya mfululizo wa mashauriano na bodi ya klabu hiyo huko Entebbe Uganda, akitajwa kama mtu wa msimu, binafsi akieleza kuwa anajisikia kuheshimiwa sana na kuwa na manufaa kwa jamii na kutambulika kwa jitihada zake kusaidia.
Msanii huyo amefanikiwa kuyagusa maeneo yote 6 muhimu ambayo huzingatiwa na klabu hiyo katika kuisaidia jamii, ikiwepo kutangaza amani, kupambana na magonjwa, kusaidia upatikanaji wa maji safi, kuokoa maisha ya wakina mama na watoto, kusaidia elimu na kukuza uchumi wa ndani.