Jumatano , 10th Sep , 2014

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Bobi Wine amesitisha mkataba wa kufanya kazi na meneja wake wa muda mrefu ambaye anajulikana kwa jina Labeja Lawrence, na kufafanua kuwa hatua hii haijatokana na tatizo lolote kati yao.

msanii Bobi Wine akiwa na meneja wake Labeja Lawrence

Kufutia maamuzi haya, Bobi Wine amesema kuwa, shughuli zote ambazo
zitahitaji kumhusisha yeye, hazitahusisha makubaliano yoyote yatakayofanyika na Lawrence.

Bobi Wine amesema kuwa, Lawrence anabaki kuwa mmoja wa wanafamilia kwake, kaka na pia rafiki huku akimshukuru kwa kuweza kufanya naye kazi kwa muda wote ambao wamekuwa pamoja.