Alhamisi , 24th Apr , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Bobi Wine baada ya kumaliza vizuri sikukuu ya pasaka, ameamua kuwakumbuka wagonjwa na akina mama wajawazito kwa kutembelea kituo cha afya cha Nakasongola huko Kampala na kutoa misaada mbalimbali.

Bobi Wine

Katika ziara hii, Bobi Wine kwa kushirikiana kwa karibu kabisa na Barbie mke wake, kati ya mambo mengine wameweza kugawa vyandarua vya kutosha kwa wagonjwa na wajawazito hawa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusaidiana na serikali ya nchi hiyo kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Msanii huyu amechukua hatua hii pia ikiwa ni kurudisha shukrani kwa jamii hasa baada ya kufanya onesho lenye mafanikio makubwa katika ufukwe maarufu wa One Love anao umiliki yeye mwenyewe nchini Uganda.

Tags: