Bob Junior
Bob Junior amefunguka kuwa sababu za kuachana na wapenzi wake wengi kwa muda mfupi ni kuendana ambapo amesema,
''Mahusiano yakianza yanakuwa na nguvu kubwa, mimi ninachoangalia huwa kuna Bob Junior na Raheem kwa hiyo unakuta wanawake wengi wengi wanaingia kumpenda Bob Junior kwa sababu ni staa na wala sio Raheem ndio maana unakuta mahusiano yanavunjika".
Aidha Bob Junior amezungumzia suala la kuwa na mahusiano na staa wa filamu Kabula kwa kusema ni dada yake, rafiki yake hajawahi hata kum-kiss na amesema Kabula amebadilika amekuwa mtu wa dini na amemtanguliza Yesu mbele.
Pia Bob Junior ameeleza kuwa amekuwa kimya kwa sababu alimua kusoma kwa siri nchini Finland alipo baba yake, na amefanya hivyo kwa manufaa ya familia yake, wazazi wake na kizazi chake cha baadaye.