Jumanne , 22nd Sep , 2015

Baada ya mwezi kupita tangu kutoka kwa ngoma yake ya kimataifa ya 'We Get It On' , staa wa muziki Black Rhyno ameeleza matunda ambayo rekodi hiyo imeleta katika muziki wake ikiwepo kueleweka zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Staa wa muziki nchini Black Rhyno

Rhyno ameieleza eNewz kuwa, producer wa kimataifa wa kazi hiyo akivutiwa kuja nchini kufanya ziara ambapo kwa sasa kazi hiyo inaendelea kupeperusha jina lake katika kipindi hiki ambapo ametulia kupisha upepo wa uchaguzi kabla ya kushambulia tena jukwaa.

We Get It On ikiwa ni project yake ya kwanza na kubwa kimataifa ambayo pia imefungua milango ya kolabo nyingine kubwa za kimataifa atakazoziweka wazi hivi karibuni.