Tukio hili lilienda sambamba na tukio la kukata keki kwaajili ya kuashiria miaka 3 ya Bongo Movie Unity.
Kati ya mambo makubwa yaliyotokea katika sherehe hii, ni kutuzwa kwa waigizaji, wakiwepo Marehemu Steven Kanumba, Mzee Kipara na Juma Kilowoko 'Sajuki' kutokana na mchango wao katika tasnia ya filamu nchini Tanzania.
Katika tukio hili pia baadhi ya wasanii wa filamu akiwepo Irene Uwoya na Jackline Wolper walijipatia shavu la kuwa mabalozi wa kinywaj/bia maarufu kwa kipindi cha mwaka mmoja, shavu ambalo limeambatana na kitita cha shilingi milioni moja kwa kila balozi.