
Msanii wa Muziki nchini, Billnass.
Billnass amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuvaa koti ambalo halikuwa saizi yake, hali iliyopelekea mashabiki na baadhi ya mastaa kumshambulia na kumsema kwamba yeye ni mmoja wa wasanii ambao hawajui kuvaa.
"Kila mtu ana namna yake ya kupima mavazi, kwamba huyu ni bora kwenye kuvaa au huyu sio bora ila mimi siwezi kujizungumzia kwenye eneo hilo na huwa navaa kile kitu ambacho nakihisi na kukipenda, kikubwa ni kuwa tofauti tu" amesema Billnass.
Aidha Bilnassa ameongeza kuwa, "Hakuna kitu ambacho navaa kabla ya mimi kujitazama, kuona kama natokanacho vipi kwa mimi na mtazamo wangu naona nipo sahihi kabisa na wala siwezi kutishika na comments za watu kwa sababu kila mtu ana mawazo yake, kuna muda unatakiwa uwe tofauti, uwe wewe na hatuwezi kufanana wote" ameongeza.