Msanii mkongwe wa filamu Bibi Mwenda na Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara
Akizungumza hilo mbele ya Camera za EATV & EA Radio Digital, baada ya Haji Manara kusema wachezaji wa Yanga ni wa kuokota Bibi Mwenda amesema
"Kwanza tumewafunga moja tu ili liliwatie hasira, tulitaka kumfundisha adabu Haji Manara kwa sababu anabwabwaja sana na anazungumza maneno mengi, aingie uwanjani aone ugumu wa mpira sio kuongeaongea"
"Anasema sisi tunaokota wachezaji kumbe yeye ndio anaokota sasa na kimbembe amekiona juzi, nawahusia wana Yanga wote Tanzania kwamba tumeshawafunga hapa Dar bado kule Kigoma" ameongeza
Mengine zaidi aliyoyazungumza tazama hapo chini kwenye video.




