Jumatatu , 4th Jan , 2016

Msanii Beyonce Knowles amepata dili la kuandika na kuigiza filamu ya maisha ya mwanamke wa Afrika Kusini Sara 'Saartjie’ Baartman, ambaye alifanywa maonyesho nchini Uingereza na Ufaransa wakati wa ukoloni kutokana na kuwa na makalio makubwa.

MJUE SARA BAARTMAN

Sara 'Saartjie’ Baartman alizaliwa mwaka 1789 katika eneo la mto Gamtoos ambalo kwa sasa linajulikana kama Eastern Cape nchini Afrika Kusini, kutoka kwenye familia ya wafugaji ya jamii ya Kho Khoi.

Sara alikulia kwenye shamba la mkoloni ambalo familia yake ilikuwa ikifanya kazi, mama yake alifariki akiwa na miaka miwili, na baba yake ambaye alikuwa mfugaji alifariki akiwa na umri wa usichana, na aliolewa na mwanaume wa Khoi Khoi ambaye alikuwa mpga ngoma na kupata mtoto mmoja aliyefariki baada ya kuzaliwa.

Kutokana na kukua kwa ukoloni Wareno walikuwa na mgogoro na Wakhoi Khoi na kulazimishwa kufanya kazi. Alipofika miaka 16 mume wake aliuawa na wakoloni wa Kireno, na yeye aliuzwa kama mtumwa kwa mfanya biashara Pieter Willem Cezar ambaye alimchukua mpaka Cape Town na kuwa mfanyakazi wa ndani wa kaka yake na kupewa jina la Kireno la ‘Saartjie’

On 29 October 1810, Sara inadaiwa alisaini mkataba na baharia wa meli ya Uingereza William Dunlop ambaye pia alikuwa rafiki wa Cezar na kaka yake Hendrik. Mkataba wake ulionyesha anatakiwa kusafiri na Hendrik Cezar na Dunlop hadi England kufanya kazi za ndani na kutoa burudani, akipewa sehemu ya mapato yatakayotokana na kuburudisha huko na atarudi Afrika kusini baada ya miaka mitano.

Taarifa zinasema kuwa Sara alikubali kusaini mkataba huo kwa kuwa hakuwa na elimu hivyo hakuwa na ufahamu, na pia familia ya jamii zake haikujua kuandika hivyo kukosa kumbukumbu, pia familia ya Cezar ilikuwa kwenye matatizo ya kiuchumi hivyo walimtumia Sara kuwaingizia kipato.

Umbile la Sara la kuwa na makalio makubwa liliwashangaza Waingereza ambao walijiona wana mamlaka. Dun lop alitaka Sara kuwa kama bidhaa ya maonyesho, hivyo alipelekwa London na kuwekwa kwenye eneo la Piccadilly, mtaa uliokuwa na vitu vingine vya kushangaza kama “the ne plus ultra of hideousness” na “the greatest deformity in the world”.

Waingereza wake kwa waume walilipa ili kumuona Sara akiwa nusu utupu, akiwa kwenye 'cage' na kugeuka kuwa kivutio kikubwa kwa watu kutoka sehemu mbali mbali.
Akiwa na Dunlop kampeni dhidi ya biashara ya utumwa ilianza kushamiri na matokeo yake mwajiri wake alifoji hati iliyoonyesha imesainiwa na mwenye sara ikikubali kufanya biashara hiyo na kwamba alikuwa hadhulumiwi haki yake kama inavyodaiwa.

Baada ya miaka minne mnamo September 1814, alisafirishwa kwenda Ufaransa kwa mfanya biashara Reaux aliyekuwa akifanya maonyesho ya wanyama, alimtumia Sara kufanya maonyesho nchini Ufaransa na kuingiza pesa nyingi kwa kutumia mwili wa Sara. Baadae alianza kumuonyesha akiwa kwenye 'cage' na mtoto wa kifaru, huku akitakiwa kukaa kama wanyama akiwa mtupu kabisa na kuficha sehemu zile ambazo haziruhusiwi kuonyesha kiutamaduni, na kupewa jina la utani la “Hottentot Venus”

Uwepo wake ulimvutia mtaalamu wa mambo asilia George Cuvier na kumuomba Reaux iwapo atamruhusu kumfanyia utafiti Sara wa kisayansi kitu ambacho alikubali, na mwezi Machi 1815 Sara alitumiwa kama French anatomists, zoologists na physiologists., na kuja na hatma kuwa Sara ni muunganisho kati ya wanyama na binadamu.

Sara Baartman alifariki mwaka 1816 akiwa na miaka 26, huku ikiwa haijafahamika kama alifariki kutokana na ulevi, ndui ama nimonia. Cuvier alichukua mwili wake kutoka kwa Polisi na kuukata kisayansi, akachukua ubongo na viungo vya uzazi na kuviweka kwenye chupa na kuvipeleka kwenye jumba la mambo ya kale ( museum ) ya binadamu mpaka mwaka 1974
Habari za Sara zilisambaa zaidi mwaka 1981 baada ya Stephen Jay Gould kuandika kitabu chake cha 'The Mismeasure of Man' ambacho kiliongelea masuala ya sayansi ya rangi ( racial science).

Kufuatia ushindi wa chama cha ANC nchi Afrika Kusini chini ya Rais Nelson Mandela, aliitaka serikali ya Ufaransa kurudisha ka mabaki ya Sara ili aweze kuzikwa nchini humo, kitendo kilichochukua miaka 8, na hatimaye mwaka 2002 mabaki ya mwili wa Sara yalirudishwa Afrika Kusini na kuzikwa, na kutangzwa kuwa tarehe 9 Agosti ni siku ya wanawake nchini Afrika kusini.

Sara alizikwa katika eneo la Hankey huko Eastern Cape

Sara 'Saartjie’ Baartman