Jumatano , 28th Apr , 2021

Ni Headlines za msanii Miss Bella kutoka kundi la 'Scorpions girl' amesema wasanii ambao wanafanya kiki wapelekwe Mahakamani na wakikutwa na hatia basi wakafungiwe gerezani moja kwa moja.

Msanii Miss Bella

Miss Bella amesema sheria ifuate mkondo wake kwa mtu anayefanya kiki au vitu visivyo na maadili mitandaoni kusiwe na haja ya kuchelewa apelekwe Mahakamani ili hukumu itoke afungwe.

"Msanii anafanya tukio leo anapelekwa mahabusu ila kabla ya saa 24 unamkuta nje, kwa hiyo hata wengine wanapata nguvu ya kurudia, sheria ifuate mkondo wake kwa uthibiti zaidi kama mtu anafanya kosa apelekwe Mahakamani moja kwa moja afungwe, ningeishauri Serikali kama inatakiwa itoke hukumu itolewe haina haja ya kuchelewa" ameeleza Miss Bella

Pia amesema kitendo hicho kikifanyika itakuwa inatoa somo kwa wasanii wanaochipukia na wanaotaka kuwa wasanii kuogopa kufanya vitu vya vilivyo kinyume na maadili ya Tanzania.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.