Alhamisi , 7th Aug , 2014

Msanii wa muziki Bebe Cool wa nchini Uganda, ameonesha sapoti yake katika michezo nchini humo, baada ya kutoa nafasi ya bure kwa washindi wa medali katika michezo ya Commonwealth, kuhudhuria onesho lake Ijumaa hii.

msanii Bebe Cool wa nchini Uganda

Bebe Cool ametoa nafasi ya meza moja ya watu Muhimu kabisa, yaani VIP bure kabisa kwa wachezaji hawa watano ambao wameiletea sifa nchi yao kupitia michezo hii.

Hatua hii ya Bebe Cool imegusa mioyo ya wengi kutokana na kuonesha kujali na kutumia nafasi yake kusapoti fani nyingine za burudani, hususan hii ya michezo.