Jumatano , 15th Jul , 2015

Katika kuonesha kuwa anapenda kupata umaarufu zaidi kila siku mwanamuziki Moses Ssali maarufu kama Bebe Cool amesema yeye ni moja wa wasanii wenye furaha mno nchini Uganda.

staa wa muziki wa nchini Uganda Bebe Cool

Furaha hiyo ya Bebe Cool inatokana video yake kuchaguliwa kuwania tuzo ya video bora nchini Afrika Kusini iliyobatizwa jina 'Love You Everyday'.

Akiongea katika tamasha la Big Mike Bebe Cool amewahakikishia mashabiki wake na wananchi wa Uganda, kuwa anaamini atarejea nyumbani na tuzo hiyo na kuomba kuungwa mkono na kila mtu.