Kundi la BBK BOYS
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo Mwenyekiti wa kundi hilo Emmanuel Salehe amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wanaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono kwa kuwa imani yao ni kwamba wanaibuka na ushindi.
"Tupo makundi 6 ila sisi mazoezi yetu ni babu kubwa, tunafanya mazoezi kwa masaa 8 kila siku lengo likiwa ni kuwa tofauti na wenzetu, tumejipanga sana na maelekezo ya jaji tumeyazingatia vizuri hivyo watu wajipange kuona burudani ya aina yake" Amesema Emmanuel.
Kwa upande wake mmoja wa wanakikundi hicho Johnson Sanga amesema maisha yake na kikundi hicho kwa asilimia kubwa ratiba ni kazi za sanaa na umoja walionao umewezesha kuwa kama familia na kusaidiana katika maisha.
Shindano la Dance100% mwaka huu linafikia tamati Jumamosi hii tarehe 24 katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Vodacom na Cocacola na kuoneshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni.