Ijumaa , 14th Oct , 2016

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Bw. Godfrey Mngereza ameisifia EATV kwa kitendo cha kuandaa 'EATV Awards' na pia kuipongeza kwa hatua yake ya kuwatumia wasanii waliojisajili katika baraza la sanaa la taifa BASATA.

Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mngereza

eNewz ilizungumza na Mngereza na alisema kuwa anaipongeza sana EATV kwa kwa kitendo cha kuweka sharti kwa wasanii watakao wania tuzo kuwa ni lazima wawe wamepitia kujisajili kwenye baraza la sanaa (BASATA) na sasa imesababisha wasanii wengi kukimbilia kujisajili.

"Nawapongeza kituo cha EATV kwa kuanzisha EATV AWARDS pia nawapongeza kwa hatua ya kutangaza kuwa ni lazima kwa msanii kujisajili na baraza la sanaa la Taifa ndipo ataweza kuingia katika kinyang'anyiro hicho, hiyo imekuwa nzuri na imeleta muamko mkubwa kwa wasanii ambao bado walikuwa hawajajiandikisha kujiandikisha ili waweze kutambuliwa rasmi kama wasanii halali wa kitanzania" Alisema Mngereza.

Hata hivyo alimalizia kwa kusema ni muhimu kwa wasanii ambao bado hawajajisajili katika Baraza la Sanaa la Taifa wakajiandikishe ili kuweza kutambuliwa rasmi na baraza hilo.

Tags: