Jumanne , 18th Aug , 2015

Baadhi ya wasanii wengi wa muziki nchini wamekuwa wakiiga miondoko ya Kinigeria ili kuweza kwenda na wakati lakini si kwa msanii Barnaba ambaye amediriki kulaumu baadhi ya wasanii kutokuwa imara katika kukuza asili yao ya muziki.

staa wa muziki wa bongofleva nchini Barnaba

Barnaba amekuwa ni msanii wa muziki ambaye kwa miaka mingi aliyokuwa akianza kuimba na kupiga ala za muziki ameiambia eNewz kuwa ni vyema wasanii watambue kuwa wanapoteza uasilia wa muziki wa nyumbani huku akimwagia sifa mwanamuziki Christian Bella kwa kuweza kumudu kubakia katika uasili wa muziki wake kwa miaka mingi.