Jumanne , 2nd Aug , 2016

Mkongwe wa Rap Bongo aliyewahi kufanya vizuri katika miaka ya nyuma Bandago amesema kwa sasa anajihusisha zaidi na matango (Voice over artist) kwa kuwa muziki bado haujamlipa vizuri.

BANDAGO

Akipiga story ndani ya eNewz Bandago amesema “ kwa sasa nafanya saana matangazo na voice over na ni vitu vinavyoniweka mjini'.

Lakini bado kutokana na mapenzi yake katika muziki amewaahidi mashabiki wake kuachia album mbili zitakazoongezana hivi karibuni.