Mozeh Thomas amesema hakuwa na haraka ya kutoa nyimbo nyingine ila alienda chimbo kwanza kujipanga zaidi
"Sikutaka kukurupuka iliniladhimu kuwekeza mda wa kutosha, ili niweze kuonesha ukomavu na mabadiliko makubwa" amesema Mozeh

Pia amesema hivi karibuni anatarajia kuachia wimbo wake mpya unao itwa SOLEMBA hivyo mashabiki waliokuwa wakihoji kuhusu ukimya wake amewataka kuondoa hofu.
"Now mziki ni biashara kubwa hivyo unatakiwa kufikiria vitu vikubwa ili uweze kushawishi wateja wako waeendelee kununua bidhaa kutoka kwako. Hivyo naahidi ujio huu mpya utakuwa mkubwa,uongozi wangu umeamua kuwekeza katika muziki wangu Punde watu watarajie Video nzuri kutoka kwangu"
Mozeh Thomas alitamba na wimbo wake wa umebadilika ambapo nyimbo yake ilikuwa ni moja kati ya nyimbo zilizofanya vizuri katika tasnia ya Bongo fleva
