Jumapili , 2nd Jun , 2024

Sabi Girl Ayra Starr anasema moja ya kitu anachokifurahia kutimiza miaka yake 21 mwaka huu ni kukutana na staa wa muziki na mfanyabiashara Rihanna jijini London Uingereza.

Picha ya Ayra Starr na Rihanna

Ayra Starr anasema kukutana na Rihanna kumemtia uchizi/wazimu kwa sababu ni msanii aliyekuwa anamtazama, kumsikiliza na hakuamini kama ipo siku atakutana naye.

"Kutana na Rihanna ni ukichaa sana: Msanii niliyekua naye namuangalia, kumsikiliza. Kamwe haufikirii kuwa siku moja utakutana na kuwa mmoja wa wasanii wake anayekupenda na ataenda kukupenda" - amesema Ayra Starr.

Ayra Starr ameachia Album yake mpya ya 'The Year I Turned 21' ambapo anasema alikuwa anajua ipo siku atakuja kuwa Star kupitia muziki au kitu chochote.