Jumanne , 14th Apr , 2015

Msanii wa muziki Avril kutoka nchini Kenya amechaguliwa kuwa msemaji wa kampeni iliyopatiwa jina la I Am Beautiful, yenye lengo la kuwarejeshea imani na nguvu wanawake na watoto wa kike juu ya uzuri walionao.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Avril

Kampeni hii imekuja kufuatia wimbi la mawazo hasi na kukosolewa kwa kundi hilo katika jamii kwa sehemu kubwa, hatua
ambayo imechangia kuwafanya wajisikie wanyonge na watu wa kukandamizwa kila siku.

Avril amechaguliwa katika nafasi hiyo kutokana na nafasi yake ya juu kisanaa akiwa kama mwanamke, akiwa amepitia changamoto na uzoefu mbalimbali kufika mahali alipo, ujuzi ambao atautumia kuhamasisha wanawake wengine katika jamii.