Pichani ni msanii msanii Amber Lulu na mfanyabiashara wa magari Uchebe
Akiijibu post hiyo kupitia mtandao huo huo wa Instagram Amber Lulu ameandika kuwa "Uchebe tuheshimiane usilete miamko yako nitakuvurugaa, mambo ya kijinga sitaki kama unatafuta kiki sio kwangu, mama kijacho hiyo mimba umenipa wewe kaa kwa kutulia kaka koma tena koma, nina mnyamwezi wangu halafu namuelewa kichizi so please".
Kwa muda mrefu sasa msanii huyo wa BongoFleva anadaiwa kuwa na ujauzito lakini yeye mwenyewe bado hajaweka wazi kama kweli ni mjamzito na haijajulikana ni nani aliyempa ujauzito huo.



