Jumatatu , 27th Aug , 2018

Rapa kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amedai haitokuja kutokea maishani mwake, kuacha kurap labda kifo ndio kiwe sababu ya yeye kumtenganisha na muziki.

Joh Makini

Joh Makini ametoa kauli hiyo leo Agosti 27, 2018 alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha PLANET BONGO kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema amekuwa mzito kutamka neno kustaafu muziki kutoka na yeye kupenda kuimba.

"Kufanya vitu vingine tofauti katika maisha hilo ni muhimu kabisa, lakini kufikiria kuacha muziki sijui, kwasababu na kuwa mzito sana kusema itafikia siku ntashindwa kurap ?, sijui ila napenda muziki sana", amesema Joh Makini.

Pamoja na hayo, Joh Makini ameendelea kwa kusema "endapo ikitokea nikiacha kurap na kutoenda studio lazima ntakuwa kwenye mzunguko wa kufanya vitu vingine na muziki pia. Sioni sababu ya kuacha muziki labda kifo ndio kitanitenganisha lakini sio kitu kingine".

Wasanii wengi wanakuwa kwenye wakati mgumu pindi wanapoulizwa kuhusu kuachana na muziki, kutokana na baadhi yao kufanya muziki kama kazi na starehe hivyo kuwawia vugumu kuachana na vitu hivyo kutokana na mazoea.

Mbali na hilo, Joh Makini amesema kwa sasa muziki wa hiphop nchini unalipa kwa kiasi kikubwa, tofauti na ulivyokuwa zamani huku akiwarushia dongo wasanii wanaolalamikia kuwa yawezekana wao wenyewe hawajajipanga katika kutoa kazi nzuri ndio maana wanayumba.