
Kushoto ni Nandy alivyomkaribisha mgeni wake na kulia ni msanii ni Billnass
Billnass ameyasema hayo kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, baada ya kuulizwa alichukuliaje suala la mpenzi wake kushambuliwa mitandaoni kuhusu suala la vyombo.
"Kiukweli mimi kwa maisha niliyokulia, familia niliyotoka, mitaa niliyokulia kuna vitu vingi sana sivijui, hata haya mambo ya vyombo gani sijui ni vitu ambavyo mimi sijui, nimekua kwenye mazingira ya nyumba ya chumba kimoja kisha viwili kwahiyo hata kuwa na meza na sehemu ya kulia ni ushindi, vyombo siyo vitu navitazamia hata baada ya kuona hivyo nina vitu vingi sana vya kuvifikiria kuliko hivyo vitu vidogo vidogo", amesema Billnas
Tazama video hapa chini