Ijumaa , 13th Mei , 2022

Album mpya ya 'Mr. Morale & The Big Steppers' ya Kendrick Lamar imetoka baada ya kuwa kimya kwa miaka mitano tangu alipoachia album yake ya mwisho ya 'Damn'.

Kendrick Lamar na familia yake kwenye cover ya album

Album hii ina jumla ya nyimbo 18 na collabo za wasanii kama Summer Walker, Ghostface Killah, Baby Keem, Kodak Black na Blxst.

Katika cover ya album anaonekana Kendrick Lamar akiwa amembeba binti yake wa miaka miwili, pia mchumba yake Whitney Alford naye anaonekana akiwa na mtoto wao mchanga aliyezaliwa hivi karibuni.