
A.K.A
Star huyo kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter amewaonyesha mashabiki wake kuwa anashangaa kukutana na taarifa kama hizo, hatua ambayo inadhihirisha kuwa si habari za ukweli, licha ya vyombo vingi kunukuu na kusambaza habari hiyo.
Vilevile star huyo ameweka wazi kuwa hafahamu chochote juu ya taarifa za mpango wa kufanya show ya kujaza uwanja mkubwa wa FNB huko Soweto ambao kampeni yake inaendelea kusambaa mitandaoni baada ya tukio la hasimu wake Casper Nyovest kufanikisha show yake iliyojaza uwanja mkubwa kama huo hivi karibuni.

