Alhamisi , 8th Mei , 2025

Msanii abigail chams ameweka historia mpya kwa kutajwa katika kipengele cha Best New International Act kwenye Tuzo za BET 2025, Kwa mara nyingine tena, Tanzania inang'aa kimataifa kupitia sauti yake ya kipekee

Pichani Ni msanii Abigail Chams

Abigail anazidi kuthibitisha kuwa kizazi kipya cha wasanii wa Bongo kina nafasi halali kwenye jukwaa la dunia,kutajwa kwake si tu ushindi binafsi, bali ni ushindi kwa muziki wa Tanzania, wasanii wachanga, na wasichana wote wanaoota kufikia ndoto zao kubwa.

 

Abigail Chams anaungana na wasanii kama Alikiba,Diamond Platnumz,Rayvanny ambao wamewahi kuwania tuzo hizo na wote walifankiwa kuzitwaa kulingana na vipengele walivyopendekezwa