Alhamisi , 1st Jul , 2021

Baada ya mapinduzi ya teknolojia kuingia nchini na wasanii kuanza kufanya video za nyimbo zao, wengi wao walionekana kupiga hatua zaidi na kuongeza wigo wa kuzitangaza kazi zao  baada ya kuanza kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya Tv ndani na nje ya nchi.

Picha ya wasanii TID, Fid Q na Alikiba

Licha ya video za muziki kuwa na faida lukuki ila kuna baadhi ya nyimbo za Bongo Fleva ambazo ni kali na zilifanikiwa kufanya vizuri sokoni lakini hazikufanyiwa video.

 Baadhi ni;

1.My Everything – Alikiba.
2.Chochote Popote – Joh Makini.
3. Mwanza Mwanza – Fid Q.
4.Mb Dogg – Akili yangu.
5.Girlfriend – TID alimshirikisha Jaymoe.