Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

VIDEO: Mwanafunzi ajirusha ghorofani

Jumatano , 28th Jun , 2017

Mtoto anayedhaniwa kuwa ni mwanafunzi wa  shule ya DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam amejirusha kutoka ghorofa ya nne mpaka chini huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika haraka.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke,  Andrew Satta amekiri kutokea kwa tukio hilo ingawa taarifa hizo zipo kwenye mitandao na hazijafikishwa kituoni hapo, lakini tayari wameanza kufuatilia ili kubaini nini chanzo cha cha tukio hilo.

"Ni kweli tumeona hilo tukio hata sisi kwenye mitandao ya kijamii lakini bado hatujapata taarifa za awali na tukio bado halijaripotiwa polisi. Sisi tumechukua hatua za kuanza kufuatilia na tukishafahamu tutaweka wazi" alisema Kamanda Satta.

MUENDELEZO

Meneja wa shule ya DYCCC (jina halijafahamika) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukanusha kwamba mtoto huyo siyo mwanafunzi wa shule hiyo na kwamba alikwenda kusherehekea sikukuu ya Idd kwani ni utaratibu wa wa shule hiyo kuombwa uwanja kwa ajili ya sherehe kila mwaka.

"Nipo nje ya Dar es salaam, lakini anayeonekana kwenye hizo video si mwanafunzi wa shuleni kwetu. Ni mtoto ambaye ametoka Morogoro na kuja Dar es salaam kwa ndugu zake. Alipofika alijumuika na wenzake kusherehekea sikukuu. Sasa kwa tukio hili waandaji watakuwa na majibu mazuri kuliko sisi, kwa sababu wao huwa wanatuomba uwanja na sisi tunawapatia. Lakini mtoto aliokolewa yupo salama na wazazi wake" alisema Meneja wa shule ya DYCCC.

Hata hivyo jina na umri wa mtoto huyo bado havijafahamika. 

Tazama video zaidi ya tukio hilo.

 

 

HABARI ZAIDI

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji