Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Daniel Kalinga
Akizungumza leo katika kipindi cha Supa Breakfast Afisa Uchaguzi kutoka, NEC, Daniel Kalinga, amesema kuwa wale ambao hawana kadi ya mpiga kura wazingatie utaratibu uliotolewa na tume hiyo ikiwemo matumizi ya pass ya kusafiria, leseni na kitambulisho cha NIDA.
"Mambo muhimu ambayo mwananchi anapaswa ayazingatie na ayajue ni ahakikishe anaanda kadi ya mpiga kura, mpiga kura ataenda yeye mwenyewe na kadi ya mpiga kura katika kituo cha kupigia kura alichojiandikisha” amesema Daniel Kalinga
Aidha Kalinga amewashauri wananchi wanaotarajia kupiga kura ambao kadi zao zina matatizo waweze kutumia vitambulisho vilivoruhusiwa na Tume ya uchaguzi kuepuka matatizo.
"Kama kadi yampiga kura picha imefutika, majina hayaonekani basi nashauri mtu aweze kutumia utambulisho mwingine ili aweze kupata haki ya kupiga kura kwasababu akienda kituoni na kadi imefutika wasimamizi hawatoweza kumtambua" amesema Daniel Kalinga
Hata hivyo kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wananchi wataruhusiwa kupiga kura katika eneo walilojiandikisha kwa ajili ya upigaji kura na si vinginevyo huku wakitakiwa kufika na vitambulisho vitakavyowawezesha wasimamizi kuwatambua.