Jumapili , 4th Jul , 2021

Wizara ya Afya kupitia kwa Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi, imeeleza kuwa tayari muongozo wa kuingiza chanjo ya ugonjwa wa Corona nchini umekamilika na chanjo itaingizwa na watu watachanjwa kwa hiari lakini hawataruhusiwa watu kuingiza chanjo kiholera.

Makubi ameyasema hayo leo Julai 4, 2021 jijini Dodoma ambapo amesema wananchi hawatatozwa fedha ili kupata chanjo.

''Muongozo wa kuingiza na kutoa chanjo umekamilika na mtu atachomwa kwa hiari yake na chanjo zitatolewa bure. Serikali haitaruhusu uingizwajI wa chanjo kiholela na kuwatoza wananchi fedha kwaajili ya chanjo'',ameeleza Prof. Abel Makubi.

Prof. Makubi amesema wamechukua hatua hizo ili kuwakinga wananchi na sio kusubiri hadi hali iwe mbaya ndio hatua zichukuliwe.

''Sisi kama serikali hatuwezi kusubiri mpaka watu wananchi wengi waathirike, tuna wajibu wa kulinda afya ya kila mwananchi, hatuwezi kusubiri mpaka idadi iwe kubwa, kwetu serikali mwananchi hata kama ni mmoja ni muhimu kwetu,'' amesema Prof. Abel Makubi.

Soma taarifa kamili hapo chini