Shida yangu siyo viwanda - Mwijage

Monday , 20th Nov , 2017

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Charles Mwijage amedai kwamba yeye hana shida na uwepo wa viwanda vingi bali  anachohitaji ni kuwepo na viwanda endelevu ambavyo vitatoa ajira ya kutosha jwa watanzania.

Akifanya mahojiano na EATV Mh. Mwijage amesema kwamba baada ya kufanikiwa kuwafahamisha watanzania kuhusu viwanda na nchi nzima kuanza kuzungumzia viwanda sasa changamoto imekuja ya kukidhi viwanda kwa nchi nzima vyenye kuweza kuwa sifa zinazohitajika

"Unajua shida yangu siyo viwanda. Lakini ninashida na viwanda endelevu ambavyo vitawakidhi watanzania wote.  Vitengeneze ajira pamoja na bidhaa mbali mbali na zenye ubora kwenye jamii inayowazunguka, hicho ndicho kiwanda mimi ninachokitaka," Mwijage.

Aidha Waziri Mwijage amesema anapata changamoto kwa sasa baada ya kufanikisha uelewa kwa wananchi kuhusu viwanda sasa mahitaji ya viwanda yamekuwa makubwa kiasi kinachomfanya kushindwa kukidhi mahitaji ya watanzania wote.