Jumatano , 25th Jan , 2023

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemhukumu Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake wanne kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kuwakuta na hatia katika makosa mawili kati ya matatu kwenye kesi ya jinai namba 10/2022 huku wafuasi wengine wanne wakiachiwa huru

 

Mahakama imesema Mfalme Zumaridi atatumikia mwezi mmoja  katika gereza kuu la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa huku wenzake wanne wakitumikia kufungo cha mwaka mmoja nje ya gereza

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza Monica Ndyekobora amesema washtakiwa wanne waliokutwa na hatia watatumikia kifungo cha nje huku mfalme Zumaridi akitakiwa kutumikia kifungo chake katika gereza la Butimba jijinj Mwanza

Aidha hakimu Ndyekobora amesema washtakiwa wote tisa hawajakutwa na hatia ya  shtaka la shamulio la kuzuru mwili huku Zumaridi na washtakiwa wengine wanne wakikutwa na mashtaka mawili ya kuwazuia askari polisi kutekeleza majukumu yao na kumzuia afisa ustawi kufanya kazi yake