
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Zitto ametoa kauli hiyo leo Agosti 8, 2021 wakati akifungua kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya chama hicho mjini unguja chenye ajenda moja ya kujadili hali ya kisiasa nchini.
Zitto pia ameshauri kutumia watu mbadala kuhamasisha chanjo, akisema hatua hiyo itasaidia badala ya kuendelea kuwatumia watu wale waliowaaminisha wananchi kuwa hakuna corona kuwa mstari wa mbele katika mapambano hayo.
“Napongeza maamuzi sahihi ya kuruhusu chanjo iingizwe nchini ili kuwalinda wananchi wake na mfumo wa afya ambao bila kinga wengi hawataweza kujilinda lakini hatuwezi kuwa na utekelezaji bora wa sera mpya za kupambana na corona iwapo tutaendelea kuwa na sura zilezile zilizotuhaminisha kutumia njia zisizoshauriwa kisayansi,” amesema Zitto.
Ameongeza kuwa, “Tuendelee kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuepuka mikusanyiko, kuvaa barakoa na kunawa kwa maji tiririka na sabuni kila wakati pamoja na kutumia vitakasa mikono”.
Pamoja na mambo mengine Zitto amezitaka Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar zichukue hatua madhubuti za kuongeza elimu kwa wananchi ambao kwa nyakati tofauti waliambiwa hakuna corona.