
Maafa yaliyotokana na ghasia hizo
Israel imeuvamia ukanda wa Gaza kwa siku tatu mfululizo na wanajeshi wa akiba zaidi ya 100,000 wameuzunguka uzio wa eneo hilo na Israel imesitisha huduma za maji na chakula katika eneo hilo.
Aidha kwenye taarifa yake Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ametangaza kuwa nchi yake iko kwenye vita ambavyo haikuvianzisha na kusisitiza kwamba kikundi cha wanamgambo cha Hamas kijiandae kulipa gharama ambayo haitasahaulika maishani mwao na kwa maadui wote wa Israel na ni lazima Israel itashinda vita hivyo na ikishinda basi dunia nzima itashinda.