Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam, Yanga imecheza kwa kujiamini na kushambulia muda wote na kufanikiwa kupata mabao hayo pamoja ja kosa kosa za hapa na pale.
Mabao ya Yanga yamefungwa katika dakika ya 1 kwa Tambwe kuunganisha mpira wa kona, na dakika ya 56 kwa kuunganisha 'kros' ya Mrisho Ngassa.
Kwa matokeo hayo, Yanga imejiweka pazuri kusonga mbele kwani katika mchezo marudiano utakaopigwa nchini Botswana wiki mbili zijazo, Yanga itahitaji sare aina yoyote.
Kesho Azam itakuwa na kibarua kizito itakapokutana uso kwa uso na El Merreikh kutoka Sudani katika mchezo wa Kwanza wa mzunguko wa awali kuwania Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika.