Makamu wa rais wa Tanzania Dkt Gharib Bilal.
Rais wa umoja huo ambae pia ni spika wa bunge la Tanzania Anna makinda amesema mambo mengi yanayoendelea kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuhakikisha wananchi wa nchi hizo wanajua kuandika na kusoma kutokana na Elimu inayotolewa katika nchi hizo kutokukidhi mahitaji.
Naye mmoja wa wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema kushiriki kwao ni sehemu ya pekee ya kujifunza na kubadilishana uzoefu utakao saidia katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazo wakabili.
Wakati huo huo, watuhumiwa 16 wa ugaidi wamepanda kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mko wa Arusha kwa mara ya tano jana, na kumuomba Hakimu Mfawidhi Mustapher Siyani kuwatajia majina ya wapelelezi wa kesi yao ili wawajue.
Hata hivyo Hakimu Siyani amesema kuwa kwa ajili ya mazingira ya kesi hiyo, hawawezi kutaja majina ya wapelelezi na pia kesi hiyo wapelelezi huwa wanabadilika mara kwa mara.
Aidha hakimu Siyani ameongeza kuwa kesi hiyo kimsingi haina dhamana, na endapo watataka dhamana wasubiri watakapofika Mahakama kuu mara bada ya upelelezi kukamilika.