Hayo yameelezwa na walimu wanaofundisha shule za msingi jijini Dar es salaam wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani.
Wakizungumza na EATV baadhi ya walimu hao wamesema uwiano uliopo kati ya walimu na wanafunzi madarasani hauridhishi ambapo mwalimu mmoja analazimika kufundisha wanafunzi zaidi ya 90 huku uwiano stahiki ni mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 45.