Jumatatu , 13th Mar , 2023

Baraza la usalama barabarani limetoa muda hadi machi 30 mwezi huu vyombo vyote vya usafiri na usafirishaji barabarani viwe vimekaguliwa na kubandikwa stika kwani baada ya tarehe hiyo magari yote yatakayo kuwa hayajakaguliwa yatakamatwa na kufanyiwa ukaguzi kwa gharama za mmiliki

Akiongea jijini Mwanza katika ukaguzi wa maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya  usalama barabarani itakayoanza marchi 13 hadi machi 14 mwezi huu, naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo  Jumanne Sagini amesema mwitikio wa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kufanyiwa ukaguzi ni mdogo

.
Ameeleza ukaguzi wa magari utasaidia kupunguza ajali barabarani akizungumzia ajali iliyotokea Geita kuwa mataili yalikuwa yameisha muda wake na kusababisha kugharimu maisha ya watu.

Sagini amewata wakaguzi wa magari kutekeleza jukumu la ukaguzi ipasavyo na yatakayo kidhi ndio yaruhusiwe na kuondoa malalamiko yanayo tolewa na wananchi kuwa zoezi hilo ni uuzaji wa stika.