Jumapili , 27th Nov , 2016

Shirika linalojihusisha na utetezi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi Under The Same Sun, limeendesha mafunzo kwa albino nchini kuhusu jinsi wanavyoweza kukabilana na changamoto katika soko la ajira pamoja na ushiriki wao katika shughuli za ujasiriamali

Vicky Ntetema akiwa amekumbatiana na mmoja wa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini hivi karibuni

Mkurugenzi wa Under The Same Sun nchini Bi. Vicky Ntetema amesema hatua hiyo inatokana na unyanyapaa katika ajira sambamba na ukosefu wa mbinu za ujasiriamali kwa jamii ya watu wenye ulemavu ngozi.

Bi. Ntetema amesema mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yamewalenga walemavu waliofadhiliwa na shirika hilo kwani moja ya malengo ya ufadhili huo ni kuona watu hao wanapata matokeo chanya katika kile walichosaidiwa.

Kwa upande wake, mmoja wa albino hao ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Bi. Shega Mboya amesema wamekuwa wakikumbana na ubaguzi mkubwa kutoka kwa waajiri ambao huwaona walemavu wa ngozi kuwa ni kundi lisiloweza kufanya chochote.

Amesema kwa muda mrefu sasa jamii imekuwa ikiwachukulia watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa ni watu wasioweza kufanya chochote wakati ukweli ni kwamba hali haipo hivyo kwani albino akipewa nafasi anaweza kufanya mambo mazuri na makubwa kuliko mtu mwingine asiye na ulemavu.

 

________________
Kumpigia KURA msanii unayempenda kwenye #EATVAwards Bofya hapa https://www.eatv.tv/awards