
Shinzo Abe
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Tetsuya Yamagami anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya tukio hilo la kutaka kufanya mauaji.
Abe mwenye umri wa miaka 67 alipigwa risasi mbili na kuanguka chini wakati akiongea na wananchi katika kampeni.
Abe alikuwa Waziri Mkuu wa Japan kuanzia mwaka 2006 hadi 2007, kisha akaja kukaa tena kwenye nafasi hiyo kuanzia mwaka 2012 hadi 2022. Ndiyo Waziri Mkuu wa Japan aliyedumu madarakani kwa muda mrefu.