Jumamosi , 10th Feb , 2024

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amefariki dunia leo Februari 10, 2024 akiwa anapatiwa matibabau katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam.

Taarifa ya kuthibitisha kifo chake imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa kwenye ziara yake mkoani Arusha.

Itakumbukwa kuwa Lowassa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2005 mpaka 2008 alipojiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

Kufuatia kifo chake, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia hii leo.