Jumanne , 27th Sep , 2016

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi, amemuagiza Kamishna wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam, kuwafukuza kazi maafisa wote waliohusika na uuzaji wa viwanja vitatu katika eneo la Makaburi lililopo Tabata Kinyerezi, DSM

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi (Kushoto)

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutembelea eneo hilo kujionea kile alichokiita kuwa ni muendelezo wa vitendo vya utapeli na rushwa vinavyofanywa na baadhi ya maafisa ardhi pamoja na watendaji wa serikali wasio waaminifu.

Aidha, Waziri Lukuvi amewaita ofisini kwake waliouziwa viwanja hivyo, ili wampe uzoefu walionao hasa jinsi wanavyofanikiwa kununua viwanja vyenye utata yakiwemo makaburi hayo kutokana na historia ya watu hao ya kununua maeneo mengi yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya umma.