Jumatano , 8th Jan , 2020

Waziri wa Ofisi ya Tawala Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI), Selemani Jafo amepiga marufuku watoto kuzuiliwa kuandikishwa darasa la kwanza sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa.

Waziri Jafo akiwa na wanafunzi

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na  Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), jijini Dodoma ambapo amesema watoto kupata elimu ni haki yao.

"Ni marufuku kuwazuia watoto kusajiliwa kuanza Darasa la kwanza, ila wale ambao hawana vyeti vya kuzaliwa wazazi na RITA ihakikishe ndni ya miezi mtoto anapata cheti cha kuzaliwa."