
Baraza la Wazee mkoani Dodoma limeitaka serikali kuboresha huduma muhimu kwa wazee ikiwa ni pamoja na maboresho katika huduma za afya, pamoja na huduma nyingine katika jamii.
Hayo yameelezwa na baraza hilo jana mjini Dodoma na wazee hao wakati wa kikao chao na mkuu wa mkoa Dodoma Bw. Jordan Rugimbana kueleza maombi ya baraza la wazee wa mkoa wa Dodoma kwa serikali ya awamu tano kufuatia bajeti ya serikali iliyosomwa hapo jana.
Aidha mwenyekiti wa baraza hilo Mzee Job Lusinde pia ameshauri serikali kuweka utaratibu mzuri kuwapatia watoto chakula mashuleni kufuatia hali ya njaa mkoani Dodoma na hali hiyo kusababisha utoro kwa watoto mashuleni na kufanya mkoa huo wanafunzi wake kuwa wa mwisho kitaifa
Mkutano huo pia uliambatana na maombi maalum ya kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli.