Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Chang'ombe, Ruvu Sekondari, IST, Kibasila, Loyola na TEYODEN wakifuatilia mafunzo
Rai hiyo iliyolewa na mkaguzi wa elimu wilaya ya Tanga Mama Marry Matola wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kuhitimu darasa la saba katika shule ya Msingi Raskazone iliyopo jijini Tanga.
Matola amesema ni vyema sasa wazazi wakaona umuhimu na kulitilia uzito suala la kuwapatia watoto wao elimu iliyo bora sambamba na ulimwengu unavyokwenda kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia yaliyopo hivi sasa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Jamila Rashid amewaasa wanafunzi hao kuwa wasione kumaliza darasa la saba ndiyo mwisho wa elimu hivyo amewataka wajipange huko wanakokwenda katika kuhakikisha wanakuwa na malengo mazuri waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kielimu.
Sanjari na hayo amesema kuwa ushirikiano wa kutosha unatakiwa baina ya walimu na wazazi kwa ajili ya kujua maendeleo ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kusaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazosababishwa na wazazi hao.