
Akizungumza katika kituo cha afya cha Mwamashimba ambapo majeruhi wanapatiwa matibabu, Dk. Mussa Lugosi amesema walipokea miili ya watu wawili wakiwa tayari wamefariki na majeruhi watatu ambao wanaendelea kupata matibabu.
Naye mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng'wilabuzu Ludigija baada ya kufika katika kituo hicho cha afya, amesema tayari ameshaelekeza afisa madini wa mkoa huo kupita katika migodi yote na kutoa elimu ya namna ya kufanya uchimbaji salama.